Nafurahi sana kupata fursa hii kuzungumza na wadau Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO). Hii ni mara yangu ya kwanza kuzungumza nanyi wateja wetu.
Nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu katika kipindi chote cha mwaka mzima uliopita, kwa kutuamini ili tuwapatie huduma hii muhimu ya maji.
Katika mwaka uliopita DAWASCO imeweza kupanua huduma zake kwa kuwafikia wateja wapya zaidi ya 8,000 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam. Katika kipindi hicho hicho, idadi ya wateja hai imeongezeka kutoka 52,223 hadi 73,798 hii ni sawa na ongezeko la karibu asilimia 40%.
Ongezeko la uzalishaji wa maji Dar es Salaam Kwa mwaka uliopita, Shirika letu la maji limeweza kuongeza uwezo wake wa kuzalisha maji hadi asilimia 90. Wakati huo huo, wateja waliofungiwa mita wameongezaka kwa asilimia 7 kutoka wateja 22,548 wa mwaka juzi hadi 34,128. Kwetu sisi watendaji, ongezeko hili linaashiria kupungua kwa malalamiko ya wateja yanayohusu ankara za maji za kila mwezi.
Matarajio ya DAWASCO mwaka 2010
Ili kulinda mafanikio yetu ya mwaka uliopita, DAWASCO inahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwenu mwaka huu. Kwa bahati mbaya, bado uzalishaji wa maji uko chini ukilinganisha na mahitaji ya kila siku. Hadi sasa, DAWASCO imeweza kukidhi mahitaji ya wateja kwa asilimia 68 tu....More .
|