UJUMBE WA AFISA MTENDAJI MKUU.
....Inaendelea......Ndiyo maana bado maeneo mengi yanakabiliwa na migawo ya maji na presha ya maji ni ndogo. Ili kutatua matatizo haya na kuboresha huduma ya maji, DAWASCO inahitaji ushirikiano wenu katika kulipia ankara zenu, tena kulipa kwa wakati mwafaka. Kwa bahati mbaya mpaka sasa ni asilimia 40 tu ya wateja wetu wanaolipia ankara zao kila mwezi. Hii ni idadi ndogo sana ikilinganishwa na gharama za uendeshaji mitambo ya uzalishaji na kulipia gharama za uendeshaji wa Shirika lako. Ndiyo maana kwa niaba ya DAWASCO, ninazidi kukusisitizia wewe mteja wetu kulipia ankara yako bila kukosa. Nakuomba uendelee kushirikiana na DAWASCO ili kuhakikisha huduma ya maji safi na majitaka kwa jiji la Dar es Salaam inaendelea kutolewa katika ubora na viwango vinavyostahili.
Ahsanteni